Ofisi Kuu ya TAKUKURU
Hayo yamebainishwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Ilala, Christopher Myava ambapo amewataka wanachama wa vyama mbalimbali kuzingatia sheria na kuepuka vitendo vya rushwa hasa katika kipindi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Madiwani, Wabunge na Urais.
Katika hatua nyingine taasisi hiyo imewafikisha mahakamani watumishi wawili kutokea ofisi ya Mtathmini Mkuu wa Serikali kwa makosa mbalimbali ya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka yaliyosababisha hasara ya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 46.

