Msanii wa HipHip Chidi Benz
Akizungumzia sapoti ya East Africa TV Chidi Benz amesema "Tangu nimeanza kufanya vitu vyangu mwenyewe naona vinaenda, vinatokea na vinakua, napata msaada kwa watu kadhaa na wanasifia naishukuru East Africa kwa sababu vyombo vingine vinanisikilizia lakini East Africa haijawahi kuwa hivyo, heshima kwa dada yetu Regina"
Kuhusu upande wa muonekano wake wa sasa Chidi Benz amesema, hakuna msanii wa HipHop "handsome boy" kama yeye kwa sababu anavutia kwa kina dada.
"Hakuna handsome boy kwenye HipHop kama mimi, sura haijakataa ila nahisi mwili ndiyo umekataa ila sura imetangulia, halafu mimi navutia kiuhalisia tangu muda mrefu, dada zangu wananiambia u-gangster wanaiona wengine ila wao wananiona handsome boy mmoja na Gentleman"
Zaidi tazama kwenye video hapa chini.