Tuesday , 16th Jun , 2020

Rais Magufuli leo Juni 16, 2020 analihutubia Bunge la 11 katika ukumbi wa Bunge Dodoma ambapo moja ya vitu alivyovieleza ni uimara vya Jeshi la vyombo vya usalama kwa ujumla ambavyo vimefanikiwa kudhibiti vitendo vya kiharifu.

Rais Magufuli Bungeni

Katika hotuba yake, Rais Magufuli amesema, "Wakati tukiingia madarakani kulikuwa na wimbi kubwa la uhalifu wa kutumia silaha, pamoja na matukio ya mauaji kule Kibiti na kupitia Vyombo vya Ulinzi na Usalama vitendo hivyo vilikomeshwa na nipende kusema kuwa nchi yetu kwa sasa ni salama" - Rais

Aidha Rais Magufuli ameelezea namna ambavyo serikali yake imefanikiwa kuimarisha Muungano katika kipindi cha miaka mitano.

"Muungano wetu umeweza kuimarika tumewekeza kushughulikia baadhi ya changamoto za Muungano na kufikia mafanikio na makubaliano ikiwemo kuhusu suala la gharama za kushusha mizigo na pia kufuta kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na deni la shirika la umeme la Zanzibar lililokuwa likidaiwa na TANESCO, na hii yote ni katika kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar", amesema.

Pia amewashukuru marais wastaafu ambao pia wapo Bungeni. "Katika hilo ndugu zangu nawashukuru hawa viongozi wetu wakuu ambao ni mzee Mwinyi alijulikana kama Mzee Ruksa, Mzee Mkapa alijulikana kama Mzee Kweli, na Mzee Kikwete alijulikana kama Mzee wa Ari mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya".

Tazama #LIVE hotuba yake hapo chini