Mwenyekiti wa bodi ya Ligi kuu, Steven Mguto
Tamko hilo limetolewa na mwenyekiti wa bodi hiyo, Steven Mguto leo Juni 15, 2020, ambaye amesema kumekuwa na changamoto ya vilabu vingi nchini kulimbikiza madeni na kutolipa stahiki za wachezaji kwa wakati tofauti na makubaliano.
Mguto amewatoa hofu wachezaji ambao wamemaliza mikataba na vilabu vyao, lakini wameagizwa kuendelea kuvitumikia kwa makubaliano hadi Julai 31, kutokana na ligi kuchelewa kumalizika kutokana na janga la Covid 19.
Vilabu vya Tanzania vikiwemo Simba na Yanga vimekuwa vikilalamikiwa na baadhi vya wachezaji ambao hata wakiachana nao, hawalipwi pesa za usajili na hata mishahara, lakini wamekua hawapati haki kwa kuwa hakuna adhabu zinazochukuliwa.
Usikose kusikiliza #Kipenga Saa 2:00 Usiku

