
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ACP Jonathan Shana
Hayo ameyabainisha wakati akitoa taarifa ya namna ambavyo, Jeshi hilo lilivyoweza kuzima tukio la kuozeshwa kwa mtoto wa miaka 12, lilitokea katika Kata ya Mussa wilayani Arumeru na kusema kuwa matukio ya namna hiyo yamekuwa yakiwahusisha Wazee wa Mila pamoja na viongozi wa Vijiji wenye tamaa ya mali.
"Sasa ninasema kwa dhati ya moyo wangu, kamwe hatutakuwa na huruma kwa yeyote atayemuozesha mtoto wake kwa sababu ya mali na kama kuna yeyote ambaye amekwishapokea mahari kwa mtoto wake, hakika nitampeleka jela na kama kuna yeyote alikula hela ya ushenga ataitapika na kwa wananchi wa kawaida ama ndugu alikula chakula kwenye sherehe hiyo kitamtokea puani" amesema Kamanda Shana.
Tazama video hii hapa chini