Saturday , 13th Jun , 2020

Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia CHADEMA Wilfred Lwakatare, ameamua kuwaweka sawa wale waliokuwa wanahisi kwamba, yeye ameamua kukihama chama chake na kusema kuwa yeye hakufanya maamuzi hayo bali chama chake kilimfukuza.

Mbunge wa Buko Mjini, Wilfred Lwakatare.

Lwakatare ameyabainisha hayo leo Juni 13, 2020, Bungeni Dodoma, wakati akichangia hoja katika Mkutano wa 19, Kikao cha 45 na kukishukuru Chama cha Wananchi CUF kwa kuonesha dalili ya kumpokea na kumfanya ajisikie yupo nyumbani.

"Ninyooshe lugha sawa sawa sababu walifikiri mimi niliondoka, mimi sikuondoka kwenye chama changu cha zamani bali nilifukuzwa na haya yote yanayotokea ni sawa na kuuangusha Mbuyu matokeo yake, kama kuna Nyumba na Migomba lazima na yenyewe itakwenda, nikishukuru chama cha CUF na wamenisaidia kustaafu nikiwa na Plate number" amesema Mbunge Lwakatare.