
Mpira wa Premier League msimu wa 2019/20
Awamu ya kwanza ya vipimo imekuja na ripoti ya maambukizi ya watu 6 ambao ni mchezaji mmoja wa Watford na wafanyakazi wawili, kocha msaidizi wa Burnley Ian Woan na wengine wawili ambao hawajatajwa.
Vipimo hivyo ni kutoka kwa jumla ya wachezaji na Staff 748 kutoka vilabu 19 ambapo klabu ya Norwich City pekee ndio ilichelewa kufanya vipimo siku ya Jumatatui na kufanya hivyo Jumanne ambapo majibu hayajajumuishwa kwenye ripoti ya jana.
Troy Deeney
Hatu hiyo ya kuwepo kwa maambukizi hususani katika klabu ya Watford kunatoa nafasi kwa wachezaji ambao wameonesha wasiwasi na pengine kugoma kurejea mazoezini wakiamini wataambukizwa na wao kuambukiza familia zao.
Mapema jana, mshambuliaji wa Watford Troy Deeney alisema yeye hayupo tayari kurejea mazoezini kwani ana hofu kubwa ya kuihatarisha familia yake hususani mtoto wake mdogo wa kiume mwenye miezi mitano tangu azaliwe.