Jeshi la polisi mkoani Tanga limewakamata kisha kuwatia mbaroni raia wawili wa kigeni kutoka Nigeria wakiwa na zana za milipuko inayotumiwa katika vitendo vya kigaidi.
Kamanda wa polisi mkoani Tanga kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi Fraisser Kashai amesema watuhimiwa hao waliotambulika kwa majina ya Kenneth Ekeneh Luodo na Amick Bonniface Aje, wamekamatwa katika kijiji cha kigwasi kilichopo kata ya mashewa wilayani Korogwe.
Amesema watu hao walikutwa kwa mwenyeji wao aliyetambulika kwa jina la Frank ambaye alitoroka baada ya operesheni hiyo.
Amesema zana hizo ambazo pia hutumika kuvunja miamba na majengo watuhumiwa walikuwa wamezihifadhi katika mabegi, ndipo jeshi la polisi walipowakamata na kuwatia mbaroni kwa ajili ya upelelezi zaidi, huku jitihada za kumtafuta mwenyeji wao Frank zikiendelea.
Katika tukio lingine kamanda Kashai amesema mtu mmoja Michael Charles amekamatwa akiwa na risasi 39 za silaha za kivita.
Kamanda Kasha amedai kuwa mtu huyo anafanya biashara ya kuuza risasi kinyume cha taratibu na kwamba ametoka nazo Monduli mkoani Arusha kwenda mkoani Morogoro