
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa.
Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Mei 9, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama kuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwa hiyari yake kama ambavyo Jeshi la Polisi lilivyoagiza siku ya Mei 7.
"Hakuna hata mmoja aliyeripoti, inawezekana hawapo Dar es Salaam na ndiyo maana nilisema kama kuna yeyote bado yupo, na hakuna aliyepatikana pia, hatujawasaka lakini ule ulikuwa ni wito" amesema Kamanda Mambosasa.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa masaa 24 kwa Wabunge ambao wako Jijini humo, waondoke na kurejea Dodoma kuendelea na shughuli zao za Bunge na atakayekaidi basi atakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa nyakati za usiku.