Saturday , 9th May , 2020

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai, amesema kuwa Mbunge yeyote ambaye anahisi ana dalili za maambukizi ya Virusi vya Corona anafanyiwa vipimo, isipokuwa hawatangazi tu kwenye vyombo vya habari.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai.

Spika Ndugai ameyabainisha hayo, wakati akifanya mazungumzo maalum na EATV&EA Radio Digital, na kuhojiwa kwamba je wanao mpango wa kuwafanyia vipimo Wabunge wote ili atakayebainika kupata maambukizi awekwe Karantini?, ambapo Spika alijibu.

"Kila Mbunge ambaye anajihisi vibaya anafanyiwa vipimo, tunachofanya hatutangazi tu" amesema Spika Ndugai.

Tazama video hii hapa chini.