Friday , 8th May , 2020

Mbunge wa Lushoto Shabani Shekilindi, amedai kugundua dawa inayotibu ugonjwa wa Corona, ambapo kwa sasa ameikabidhisha Serikalini ili kupata uthibitisho wa Maabara.

Mbunge wa Lushoto Shabani Shekilindi

Shekilindi ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Mwandishi wa EATV / EA Radio Digital, Sangu Joseph, ambapo amesema kupitia dawa hiyo ya tiba asili ameshawatibia wagonjwa zaidi ya 30 na wote wamepona.

"Mpaka dakika hii nimeponya wagonjwa zaidi ya 30 ambao wamepona Corona kupitia dawa yangu, na nilichokifanya nimezungumza na Waziri Mkuu ambaye alinikabidhisha kwa Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, ili kuipeleka Maabara kwa ajili ya uthibitisho wa kitaalam." amesema Shekilingi.

"Endapo Serikali itakubali juu ya dawa yangu, kwa sasa siwezi kusema itakuwa gharama shilingi ngapi, hilo nitawaachia Serikali, ila lazima gharama iwepo ili kusaidia utengenezaji" ameongeza Mbunge wa Lushoto Shabani Shekilindi.

Tazama video kamili hapo chini :-