
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli
Rais Magufuli ameyabainisha hayo kupitia taarifa yake iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kusema kuwa kwa mwaka huu, sikukuu za Mei Mosi hazitafanyika ili kuepuka mikusanyiko ya watu ikiwa ni tahadhari ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
"Ndugu wafanyakazi wenzangu nawapongeza sana kwa kuchapa kazi, mimi nipo pamoja nanyi na ninatambua na natambua kazi nzuri mnayoifanya, nawaomba katika kipindi ambacho Dunia inapita katika wakati mgumu wa kukabiliana na ugonjwa wa Corona, sisi tuendelee kuchapa kazi kamwe ugonjwa huu usiwe sababu ya kurudi nyuma na kuacha kuwahudumia Watanzania, mimi naamini Mungu atatuvusha" amesema Rais Magufuli.
Aidha Rais Magufuli amewapongeza waajiri wote wa Serikali na Sekta Binafsi na kutoa wito kwao kutotumia ugonjwa wa Corona kama kigezo cha kuwanyanyasa wafanyakazi.