Thursday , 23rd Apr , 2020

Unaambiwa kwenye maisha ya sasa ili ufanikiwe unatakiwa uwe na kitu kimoja kati ya hivi viwili ambavyo ni uwezo au bahati ambavyo vitakusaidia kwenye mipango yako ya kutafuta maisha.

Msanii Alikiba

 

Sasa EATV & EA Radio Digital, imepiga stori na mfalme wa BongoFleva Alikiba na amefunguka kitu gani anachokiamini kwa upande wake kati ya bahati na uwezo katika maisha.

"Kuna muda unatakiwa kuwa na bahati, ila lazima uwe na uwezo pia kwa sababu bahati huwa inamchagua mtu, vilevile kuna watu wana uwezo lakini hawana bahati, kwahiyo tunahitaji bahati kwenye maisha yetu maana ukiwa na nguvu ya bahati hakuna hata mtu mmoja ambaye ataweza kukupa changamoto" amesema Alikiba.

Tazama mahojiano kamili hapa hapa chini.