
Hii ndiyo sehemu aliyopumzishwa, Askofu Dkt Getrude Rwakatare.
Mazishi hayo yamefanyika Alhamisi ya leo ya Aprili 23, 2020, majira ya saa 7:00 mchana na kuhudhuriwa na watu kadhaa ndani ya familia.
Baadhi ya watu walioshiriki katika ibada ya mazishi ya Askofu Dkt Getrude Rwakatare.
Mama Rwakatare alifariki Dunia Aprili 20, 2020, katika hospitali ya Rabininsia, alikokuwa akipatiwa matibabu, ambapo kwa mujibu wa mwanaye Mutta Rwakatare, alisema kuwa Mama yao alikuwa akisumbuliwa na tatizo la moyo na presha.
Kaburi la Mama Rwakatare, likiombewa.
Mungu ailaze Roho ya marehemu, Mama Getrude Rwakatare, mahala pema. Amina.