
Virusi vya Corona
Marufuku hiyo imetangazwa na Mkurugenzi anayehusika na mambo ya miradi ya Kanisa hilo nchini, Sessan Msafiri, katika ibada ya kuliombea Taifa kuondokana na ugonjwa hatari wa Corona, iliyofanyika Kanisa la Wasabato Sabasaba Tarime, Jimbo la Mara.
"Kama Kanisa kuna mambo mengi tumeyafanya ikiwemo kuzuia safari za viongozi kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine, nisisitize kuwa Tarime ikpo mkoani kwahiyo tunaweza kupokea wageni wengi kutoka Kenya", amesema Sessan Msafiri.
Pia Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa kila muumini kuweka karantini nguo anazovua baada ya kufika nyumbani akitoka kazini.