
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Katika salamu hizo, Dkt Magufuli ameelezea kusikitishwa na kifo cha Askofu Getrude Rwakatare, ambaye amesema alikuwa mcha Mungu, mwenye upendo, asiye na majivuno, aliyepigania umoja na amani na aliyeipenda nchi yake kwa dhati.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, ameonesha kusikitishwa na taarifa ya kifo cha Mama Rwakatare na kusema kuwa Bunge linaratibu mipango ya mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Rwakatare, natoa pole kwa wafiwa wote ikiwemo familia, ndugu, jamaa, Waheshimiwa Wabunge na waumini wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mwenyezi Mungu awape moyo wa umilivu na subira katika kipindi hiki kigumu" imeeleza taarifa ya Spika Ndugai.