
Sampuli za vipimo
Aidha kwa mujibu ya taarifa ya vipimo vya sampuli vya watu 1,126, vilivyochukuliwa siku ya jana ya Aprili 18, 2020, vimeleta majibu ya kwamba wote hawana maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo kati yao madereva wa malori ni 837 na waliosalia ni wale watu waliokuwa wakifuatiliwa kwa ukaribu.
Aidha mpaka sasa nchi ya Uganda haijaripoti kifo chochote cha mgonjwa wa COVID-19, tangu nchi hiyo ianze kupata maambukizi hayo.