Sunday , 19th Apr , 2020

Wizara ya Afya Zanzibar imetangaza ongezeko la wagonjwa 23 wa COVID-19, hivyo kufanya idadi ya wagonjwa kisiwani humo kufikia 58, kati yao wagonjwa 21 ni raia wa Tanzania, mmoja wa Ufaransa na mmoja wa Cuba.

Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 19, 2020 na Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohammed, na kueleza kuwa wale waliofariki walifia nyumbani, kabla ya kuchukuliwa vipimo na hivyo kufanya idadi ya vifo visiwani humo kuwa ni vitatu.

Aidha Serikali imeendelea kuwahimiza wananchi kufuata kanuni zote za afya zinazotolewa na kuwataka wale wenye dalili za ugonjwa huo, waache kujitibia nyumbani kwani kwa kufanya hivyo ni kuendelea kueneza maambuki na vifo vinavyohusiana na ugonjwa huo.