Wednesday , 15th Apr , 2020

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof Ibrahim Lipumba, amewashauri vijana ambao wanataka kuingia kwenye mahusiano kwa kusema, wachukue muda kwanza kabla ya kuanzisha mahusiano kisha watafute mahusiano ambayo yatadumu kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa Chama cha CUF Prof Ibrahim Lipumba

Akipiga stori na Big Chawa kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio ambayo inakuwa hewani kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 7:00 mchana hadi 10:00 jioni, Profesa Lipumba amesema,

"Mimi nilikutana na mama yenu Chuo Kikuu cha Mlimani, japo hatukuwa na mahusiano, ila baada ya kugombea Uraisi nikarudi nikamuoa, ni vyema katika mahusiano mchukue muda kwanza, kama kijana unahitaji mahusiano ya muda mrefu hasa kwa familia kwa sababu mnapokuwa na watoto mnapoachana watoto hukosa malezi ya wazazi wote wawili" amesema Prof Lipumba.