Wini
Akipiga stori na Friday Night Live ya EATV, Wini amesema kuwa anapenda sana kupiga picha nzuri na kuziweka mtandaoni na kusema kuwa kuhusu watu kuchanganyikiwa na picha zake ni sehemu ya kazi.
"Mimi napenda picha sana na huwa nazitumia katika kazi zangu mbalimbali kama 'Cover' za nyimbo zangu na hata 'Cover' za 'Interview' mbalimbali wanatumia hizo kwahiyo ni moja ya kazi", amesema Wini.
"Sio kwamba napenda picha za kuwatega hapana ila ni katika kuonesha kazi mbalimbali kwa sababu ninafanya kazi na kampuni mbalimbali kama wabunifu wa nguo", ameongeza.
Kuhusu ujasiriamali, Wini amesema yeye ni mkulima aliyewekeza katika zao la Zabibu lakini siyo kwamba analima mwenyewe bali amewekeza pesa.
Wini anatamba na wimbo wake unaojulikana kama 'Mandingo' ambao ameutambulisha rasmi katika FNL.