Thursday , 9th Apr , 2020

Mfalme wa BongoFleva  Alikiba, amesema alishangazwa kumkuta mrembo Hamisa Mobetto visiwani Zanzibar, kwa sababau alikuwa hajui kama ndiyo atafanya naye kazi katika wimbo wake mpya wa Dodo.

Alikiba na Hamisa Mobetto wakati wanarekodi video ya wimbo wa dodo

Akiileza hayo kwenye kipindi cha PlanetBongo ya East Africa Radio, Alikiba amesema kazi na mawazo "idea" ya kufanya video na Hamisa Mobetto ilifanywa na timu yake pamoja na uongozi wake.

"Kufanya kazi na Hamisa Mobetto ni vizuri kwa sababu ana mashabiki wengi na kuhusu kuwa "video vixen" hata mimi nilikuwa sijui, kazi na idea hiyo imefanywa na timu yangu pamoja na uongozi wangu, hata mimi nilishangazwa sana kumkuta kule Zanzibar" ameeleza Alikiba.

Aidha akizungumzia juu ya kuweka video hiyo ya wimbo wake wa dodo katika akaunti ya YouTube ya Kings Music msanii huyo amesema, "Nia na malengo ya kuweka video hii kwenye YouTube channel ya Kings Music ni kutaka kuikuza na kuitafutia wafuasi wengi kwa sababu bado inakua, hata wimbo wangu wa  mshumaa niliuweka kule".