Msanii wa HipHop Chidi Benz
Chidi Benz ameomba msamaha huo baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonyesha anazungumzia ugojwa huo kwa njia ya utani kupitia chombo kimoja cha habari kwa kusema
"Corona ni mafua ambayo yamekuwa ni mara mbili yake, watakaoathirika ni wale ambao mfumo wao wa pua utakua unashika vumbi kwa haraka ila kwa sisi Waafrika ukikamua mafua yanatoka kama keki Corona haipiti kokote"
Aidha akiomba msamaha huo Chidi Benz ameeleza kuwa "Kuhusiana na Corona ni ugonjwa ulio serious mtu yoyote asiuletee utani, mimi naomba msamaha kwa kile nilichokifanya kuhusu Ugonjwa wa Corona, ile niliongea kama utani tu ili nisichanganye watu".