
Wanandoa wakila kiapo kanisani, huku wanajikinga na ugonjwa wa Corona kwa kuvalia maski usoni
Tukio hilo la ndoa ambalo limefanyika huko New Orleans nchini Marekani, likimuhusisha bwana harusi Christopher na bibi harusi Tessa, ambao hawataisahau siku yao hiyo kwa sababu wameshea busu lao la kwanza huku wakiwa wamevalia maski mdomoni na uso mzima.
Pasta wa kanisa la French Quarter Wedding Chapel, aitwaye Rev Tony ambaye amefungisha ndoa hiyo amesema "Penzi la Christopher na Tessa ni la ukweli, kwa sababu wamechukua ujasiri wa kufunga ndoa wakati Dunia ipo katika janga la ugonjwa wa Corona ambapo wengine wamezuiliwa hadi kusafiri".
Katika kujikinga na ugonjwa huo kwenye Jiji hilo la New Orleans, tayari wameshafunga kumbi za starehe kama bar na vilabu, mikutano ya hadhara na Polisi wanafanya ulinzi kila Mitaa ili kuwakamata wale watakaoikaidi agizo lao.