Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe akiwa mahakamani
Februari 18, 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu mwandamizi Huruma Shaidi, ilimkuta kiongozi huyo na kesi ya kujibu, ambapo pia jumla ya mashahidi 10 wanatarajiwa kumtetea.
Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Kijitonyama Dar es Salaam.
Mashtaka ya Zitto yanatokana na kauli zake za kulitaka jeshi la Polisi, kutolea maelezo kwa kile alichokiita mauaji ya Polisi na raia, yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.







