Waziri wa Afya nchini Kenya, Mutahi Kagwe.
Hatua hii inakuja baada ya hii leo Machi 13, 2020, Serikali hiyo kupitia Wizara ya Afya, kuthibitisha kisa cha kwanza cha ugonjwa hatari unaosababishwa na Virusi vya Corona.
Waziri wa afya nchini humo Mutahi Kagwe, amesema kuwa mgonjwa huyo aliingia Kenya kutoka Marekani kupitia Uingereza Machi 5, 2020, ambapo kwa sasa anaendelea vizuri baada ya hapo jana kufanyiwa vipimo.
Mgonjwa huyo kwa sasa yuko katika hospitali ya Kenyatta, huku Serikali ikianzisha shughuli ya kuwatafuta watu waliokuwa naye.
