Dkt Vicent Mashinji
Dkt Mashinji ameyabainisha hayo leo mara baada ya kuachiwa huru, baada ya jana kushindwa kulipa faini yake na kupelekwa Gereza la Segerea na kuliomba Taifa kuendelea kuboresha zaidi Magereza.
"Niwashukuru sana ndugu zangu wa CCM, miaka miwili iliyopita nilipata kuwa hapo gerezani, sasa hivi kuna improvement kidogo, naomba kama Taifa tuendelee kuboresha maeneo yote tunayowahifadhi wananchi, nilitegemea kama kule nilikotoka hili suala lingekuwa la Kitaifa, lakini nimeshangazwa kuona limefanywa tu na Mkoa, najiona niko sehemu salama zaidi" amesema Dkt Mashinji.
Dkt Mashinji pamoja na viongozi nane wa CHADEMA, kutokana na kesi yao ya uchochezi iliyokuwa ikiwakabili, jana Machi 10, 2020, walihukumiwa faini ama kifungo cha miezi mitano jela na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

