Picha ya msanii Nandy
Akitoa taarifa hiyo kupitia post aliyoweka katika mtandao wa Instagram, Nandy amesema anafanyiwa vitu vya ajabu sana, watu wanamrudisha nyuma kwani idadi ya watazamaji katika video ya wimbo wake wa na nusu wanapungua.
"Nimevumilia hii siku ya nne sasa, huko Youtube kunatokea vitu vya ajabu sana sijui nini tatizo, ikifikisha watazamaji laki tisa, wanarudishwa nyuma hadi laki nane au saba, naona miujiza tu kwenye akaunti yangu, sitaki kuhukumu watu naomba watu wa ufundi wanisaidie kujua kuna nini" ameandika Nandy.


