Monday , 9th Mar , 2020

Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, amesema kuwa hana matatizo na Freeman Mbowe isipokuwa ana shida juu ya utekelezaji wa majukumu yake kwa wananchi na kwamba ataendelea kuiunga mkono kauli ya Katibu Mkuu wa CCM Dkt Bashiru Ally ya kuongoza kwa dola.

Mbunge wa Hai Freeman Mbowe na Mkuu wa Wilaya hiyo, Freeman Mbowe

Sabaya ameyabainisha hayo leo Machi 9, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, wakati akijibu tuhuma za Mbowe juu yake kuwa amekuwa akitumia madaraka yake kuunda makundi ya vijana na kwenda kufanya vurugu katika mikutano yake.

"Sina Mgogoro na Mbowe, ila yeye ana mgogoro na wanachi wake waliompigia kura kwani wamekuwa wakimuuliza maswali na yeye ana wajibu kuwa ni wahuni, aache kutafuta huruma, watu wametafsiri kauli ya Dkt bashiru tofauti lakini ukweli ni kwamba lazima utekeleze Ilani ambayo uliitumia kuomba kura na mimi nitaendelea kutekeleza" amesema DC Sabaya.

Aidha Sabaya amesema kuwa hana mpango wowote wa kugombea Ubunge kwa lengo la kuchukua nafasi ya Mbowe kwa kuwa ameridhika na nafasi aliyopewa na Rais Dkt John Pombe Magufuli.