Monday , 9th Mar , 2020

Baada ya kuwa na taarifa nyingi kuhusu uhusiano wa kimapenzi kati ya rapa Young Killer na staa wa filamu Jacqueline Wolper, huenda ikawa kweli yametimia kwani wawili hao wamethibitisha hilo katika mitandao ya kijamii.

Picha ya pozi kati ya Young Killer na Jacqueline Wolper

Kila ifikapo Machi 8 ya kila mwaka, Dunia huadhimisha siku ya wanawake, ambapo Young Killer alitumia fursa hiyo kupost picha yake akiwa pamoja na Wolper katika mtandao wa kijamii wa Instagram na kuandika.

"Yaani wewe mwanamke usiku silali, mchana Tarime, kheri ya siku ya wanawake duniani".

Baada ya muda mfupi kupost picha hiyo naye Jacqueline Wolper akaja ku-comment kwa kuandika   "Ahsante sana Erick kwa kunipenda mimi, nakupenda pia ngosha".

Kwa dalili hizo na maelezo hayo, yanamaanisha wawili hao kwa sasa wapo kwenye mahusiano ya kimapenzi, japokuwa wote walikuwa wanakana kipindi cha nyuma.