Thursday , 5th Mar , 2020

Kufuatia kampeni ya pekenyua tukufukunyue, iliyozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji imeanza kuzaa matunda ambapo mpaka sasa, wamefanikiwa kuwakamata na kuwachukulia hatua wahamiaji haramu 150 kutoka Mataifa mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji, Novaita Mrosso, ambapo amesema kuwa wahamiaji hao haramu 150 kati yao Watanzania ni 95, 25 kutoka Burundi, Ethiopia 23, CAmeroon 2, DRC 2, Comoro 1, Kenya 1 Rwanda 1 na Uganda 1.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mpaka sasa bado wanaendelea na operesheni kabambe ndani ya Jiji la Dar es Salaam, ambapo Idara ya Uhamiaji inawashikilia wahamiaji haramu 110, wakiwemo 76 ambao upelelezi wao umekamilika, ambao walikuwa wanajihusisha na biashara ndogondogo ikiwemo uuzaji wa Pipi, Kahawa, Madafu, Soda na Maji.