Rais Dkt Magufuli alivyokutana na viongozi wa vyama vya siasa nchini
Dkt Magufuli amekutana nao leo Machi 3, 2020, Ikulu ya Dar es Salaam na kufanya nao mazungumzo ya faragha na kila mmoja kwa wakati wake.
Akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yao, Maalim Seif ameeleza.
"Mimi na Mh Rais tumekutana na kubwa ni kuzungumzia mambo ya nchi yetu, ni mtu muwazi anapenda kukutana na watu na kupata mashauri ya watu, anakubali kukutana na raia wake ni jambo zuri,namshukuru amekubali tukutane tuzungumze mambo ya maslahi ya nchi yetu" amesema Maalim Seif.
Kupitia picha na video fupi zilizopigwa wakati wa mahojiano yao, zimeonesha ni kwa namna gani, Rais Magufuli alivyotekeleza agizo la Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu la kusalimiana bila kupeana mikono ikiwa ni tahadhari ya homa kali inayosababishwa na Virusi vya Corona (COVID -19).
