Tuesday , 3rd Mar , 2020

Watu kadhaa wamejeruhiwa baada ya kuzuka mapigano kati ya Jeshi la Serikali ya Somalia na wanajeshi wa Jubaland, waliofyatuliana risasi katika mpaka wa Kenya na Somalia hapo jana.

Vitu vikiteketea kutokana na mapigano hayo

Inaelezwa kuwa milipuko ya risasi ilitanda kwa masaa kadhaa huku wananchi wenye hofu,wakiiomba Serikali kuingilia kati.

Hayo yote yanajiri ikiwa imepita siku moja tu tangu Wabunge 11, ambao Sita ni kutoka Mandera, watatu kutoka Wajir na wawili kutoka Garisa ,kufanya mkutano wa kutafuta amani nchini Somalia na baadaye Serikali ya Kenya iliwakamata kwa mahojiano na kuwaachia.