
Picha ya Director Shaibu
Sasa kupitia EATV & EA Radio Digital imempata Director Shaibu, ambaye amesema hakutegemea msemo wake kama utatrend midomoni mwa watu na mitandaoni kwa sababu maisha ni magumu na wengi wao hawatoi pesa kiulaini.
"Hali ya maisha ni ngumu pia sio ngumu sana kwani inategemea na mtu anachofanya kwa upande wake, nimejaribu kuongea uhalisia ambao tupo nao, kwani tumeshajizoesha kama buku ni kiasi kidogo cha fedha, lakini sasa hivi watu wanakaza hawatoi, utashuka hadi kwenye jero na mia mbili lakini mtu bado hana au hatoi kabisa" amesema Director Shaibu.
Aidha ameendelea kusema nia ya kutoa msemo huo ni kuwahimiza vijana wawe wabunifu, waache kuomba pesa na wafanye kazi.