Thursday , 27th Feb , 2020

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, leo Februari 27, 2020, amemteua Balozi John Kijazi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGEA).

Rais Dkt John Pombe Magufuli na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.

Ikumbukwe kuwa Balozi John Kijazi ni Katibu Mkuu Kiongozi.

Aidha Rais Dkt Magufuli amemteua Mhandisi Florian Kabaka kuwa Mwenyeki wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), uteuzi wa viongozi hao umeanza jana Februari 26, 2020.