Kushoto pichani ni Emmanuel Mbasha, kulia ni Muna Love
Taarifa hizo za kuolewa na kubadilisha dini zilisambaa zaidi siku ya jana Februari 7,2020 kupitia mitandao ya kijamii, baada ya Muna Love kuomba kupumzika kutumia mtandao wa Instagram kwa muda.
Kwa Upande wa Emmanuel Mbasha amefanunua zaidi juu ya suala hilo na ametaka watu wamkome kumuuliza kwa sababu sio mume wake na anachojua kuwa Muna ni mpambanaji wa Yesu na mfanyabiashara.
"Jamani nawaomba sana naona simu nyingi na message kuhusu kutaka interview, nasema mimi sio mme wa Muna mnikome kama anaolewa nifanyeje sasa, ninachokujua kuwa Muna ni kamanda wa Yesu, mpambanaji, na mfanyabiashara. Huko ana-shoot filamu yake, msinisumbue nazima simu imekua kero msinisumbue mpigieni mwenyewe" ameandika Emmanuel Mbasha