Amber Rutty na mpenzi
Kupitia taarifa ya maandishi waliyotoa BASATA, wamesisitiza kuwa hawamtambui Amber Rutty na hajasajiliwa kama msanii hivyo wao hawawezi kumwadhibu.
''Hajasajiliwa kama msanii binafsi au msanii kutoka kwenye kikundi chochote, lakini picha hizo haziendi sawa na maadili ya Kitanzania hivyo mamlaka zinazoshughulikia mitandao ni vyema zikachukua hatua''.
Aidha BASATA imetoa wito kwa wasanii kuendelea kulinda maadili na utamaduni wa Kitanzania pamoja na kutumia teknolojia hususani mitandao kwa kujiingizia kipato na sio kuvunja sheria.
''Ni matumaini ya BASATA kuwa wasanii wote wataitumia vizuri mitandao ya kijamii na si vinginevyo''. Imemalizia taarifa hiyo.