Saturday , 11th Jan , 2020

Mvua zinazoendelea kunyesha katika mkoa wa Rukwa zimeendelea kusababisha maafa baada ya kusomba madaraja manne katika barabara ya Kasansa – Kilyamatundu inayounganisha mikoa ya Songwe, Rukwa na Katavi iliyopo bonde la ziwa Rukwa Wilayani Sumbawanga huku ikisababisha vifo vya watu watatu

Daraja lilibomoka sababu ya Mvua mkoani Rukwa

katika wilaya ya Kalambo na Nkasi mkoani humo.

Mvua hizo zilizosomba madaraja katika vijiji vya Muze, Kifinga, Lwanji na Msia vilivyopo Wilaya ya Sumbawanga imesababisha kukatika kwa mawasiliano baina ya kata na kata, kijiji na kijiji pamoja na mikoa hali iliyoleta taharuki kwa wananchi wanaoishi katika bonde hilo lenye kata 13 na wakulima wengi wa mpunga wanaosafirisha bidhaa zao katika mikoa ya jirani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo alipofanya ziara ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na maafa hayo na hivyo kuwatahadharisha wananchi kuacha tabia ya kulazimisha kupita katika njia ya maji pindi wanapoona mvua ni kubwa na hivyo kuwataka kusubiri mvua ipungue ndipo waendelee na shughuli zao.

Mimi niwaombe ndugu zangu hasa kinamama na watoto, mnapoona mvua zimekuwa nyingi maji yanaweza yakajaa wakati wowote, jihadharini msipite, acheni maji yapungue halafu mpite, lakini msiwe wabishi, mkiwa wabishi mtabebwa na mafuriko, hasa watoto wadogo hawalelewi kitu wanadhani maji kama hivi anaona kama yametulia anasema mimi nitapita tu, kwahiyo waambieni watoto nyumbani wachukue tahadhari, mkiona kuna mvua kuna mafuriko watoto wasiende kwenye shughuli zao muwazuie kuokoa maisha yao” Alisisitiza

Bonde la ziwa rukwa limeshakatika kimawasiliano kabisa kwasababu magari yanayotokea Mbeya, kule Somgwe kupitia daraja letu la Kilyamatundu pale hawawezi kufika Muze mpaka huko Katavi kama hapa hapatakuwa pameshughulikiwa kwahiyo weka nguvu kubwa sana Meneja wa TANROADS hapa ili kuhakikisha wananchi wetu wanapata usafiri wao wa kawaida ndani ya muda mfupi,