Saturday , 4th Jan , 2020

Mlinzi wa kulia wa klabu ya soka ya Azam FC, Nickolas Wadada ambaye ni raia wa Uganda, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.

Wadada (kushoto) na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'.

Awali mkataba wa Wadada ulikuwa unamalizika Julai 2021, hivyo kwa kusaini mkataba huo mpya kutamfanya aendelee kusalia hadi 2022.

Wadada amesaini mkataba huo, leo Jumamosi mchana mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin 'Popat'. 

Nickolas Wadada aalisajiliwa na Azam FC akitokea Vipers FC ya Uganda. Msimu huu tayari ameshatengeneza magoli manne na kufunga moja kwenye Ligi kuu soka Tanzania Bara.