Wednesday , 1st Jan , 2020

Homa ya mpambano kati ya watani wa Jadi Simba na Yanga imezidi kupamba moto, ambapo siku ya leo Disemba 1, 2020 msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara, amesema timu yao itaingia kama 'Underdog' ili kuwaheshimu wapinzani wao.

Haji Manara

Haji Manara amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari akiongelea kuhusu mipango ya mchezo wao dhidi  ya Yanga, ambapo Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo unaotarajiwa kupigwa siku ya Jumamosi ya Januari 4, 2020 majira ya saa 11:00 jioni katika uwanja wa taifa.

"Mechi hii sisi ndiyo wenyeji wa mechi hii, tunawaomba mashabiki wakate tiketi na kufika uwanjani mapema, hatutawacheka wala kuwadharau Yanga, wala hatuwambii wachezaji wetu wawe na mapembe,  tunawaheshimu na tutaingia kama 'underdog' kwenye mchezo huo na tutawapa ukubwa wao, mimi nitaongea baada ya mchezo kumalizika" ameeleza Haji Manara.

Aidha Haji Manara ameendelea kusema Simba wanazihitaji  alama tatu za Yanga kama walizozipata kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ndanda, pia kauli mbiu watakayoingia nayo siku ya mchezo huo ni One Touch and Three Points.