Wednesday , 1st Jan , 2020

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema mwaka 2019 ulikuwa mwaka wake wa kujifunza mambo mengi zaidi na umemuimarisha yeye kiuongozi.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo

Aidha katika salamu zake za mwaka mpya Mrisho Gambo amemshukuru Rais kwa kuendelea kumuamini kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuahidi.

Gambo ameandika "ninamshukuru Mungu nimevuka mwaka 2019 salama, ulikuwa ni mwaka wa mapito ambayo kwa kiasi kikubwa yameniimarisha kiuongozi Ni mwaka ambao umeniongezea ujasiri zaidi wa kazi, karibu mwaka 2020, ni mwaka wa kufanya kazi kwa akili na weledi zaidi. Ni mwaka wa kusimamia matokeo makubwa zaidi."

"Tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanyia nchi yetu, namshukuru pia kwa kunipa heshima mimi Mtoto wa Mama muuza UJI ya kuwa msaidizi wake kwenye ngazi ya Mkoa." ameongeza Mrisho Gambo