Tuesday , 24th Dec , 2019

heria na Haki za Binadamu (LHRC), Tito Magoti amefikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo la kutakatsha pesa shilingi Milioni 17.

Tito Magoti akiwa Mahakamani

Katika shitaka hilo Magoti amejumuishwa na wenzake Mtaalam wa Masuala Mtandao wa LHRC Theodory Giyan, ambao wote mnamo February Mosi na Disemba 17 wanatajwa kumiliki Program za Kompyuta  na baadaye kujipatika Milioni 17 ambazo si zao.

Shtaka linamkabili na Magoti na Giyani ni kuwa sehemu ya Mtandao wa kiuhalifu, pamoja na kumiliki Mtandao wa Kompyuta uliotengenzwa kwa ajili ya kufanya uhalifu.

Hakimu anayesimamia Kesi ya Magoti na Wenzake ni Janeth Mtega ambapo kesi hiyo sasa imesogezwa mbele hadi January 7, 2020 huku washtakiwa hao wakirejeshwa rumande kutokana na aina ya makosa wanayoshtakiwa kukosa dhamana.

Magoti alikamatwa Ijumaa la Disemba 20, akiwa maeneo ya Mwenge jijini Dar es salaam huku siku chache baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam akithibitisha kuwa Jeshi hilo kumshikilia Tito Magoti lakini bila kueleza sababu yake.