Thursday , 24th Oct , 2019

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi hapa nchini (TACAIDS), Dkt Leonard Maboko, amesema kuwa Serikali imeanza kutoa mwongozo wa matumizi ya dawa mpya, inayojulikana kwa jina la TLD, dawa ambayo itakuwa ikifubaza Virusi vya Ukimwi kwa muda wa miezi sita.

Hayo ameyabainisha leo Oktoba 24, 2019, wakati akizungumza na EATV, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni yake ya kibiashara zaidi na kuwasisitiza watu kujua afya zao na kuhakikisha vijana hawafanyi ngono zembe.

''Asilimia 87 tu wameshafubaza Virusi vya Ukimwi, kwamba asilimia 13 hawajafubaza Virusi vya Ukimwi, sasa hivi Wizara ya Afya nafikiri imeanza kutoa muongozo wa dawa mpya, inayofubaza virusi vya ukimwi kwa muda mfupi kwa kitaalamu inaitwa TLD, ambayo inapunguza kwa haraka sana virusi vya Ukimwi na inafubaza virusi ndani ya miezi sita tu na Wizara inaendelea kutoa muongozo wa matumizi ya hizo dawa'' amesema Dkt Maboko.

Aidha Dkt Maboko amesema kuwa kiwango cha fedha kinachotengwa na Serikali kila mwaka, kimekuwa hakitoshelezi malengo ya tume hiyo na kwamba uhitaji wao wa fedha ni kiasi cha Shilingi trilioni 1.3, fedha ambayo itaweza kwenda sambamba na mikakati waliyojiwekea.