Thursday , 24th Oct , 2019

Muigizaji na msanii wa muziki Hamisa Mobetto, amemfanyia kufuru mama yake mzazi kwa kumnunulia gari aina ya Toyota Alphard ya rangi nyeusi yenye namba D, ambayo thamani yake ni Milioni 40 za Tanzania.

Taarifa za Hamisa Mobetto kumnunulia gari mzazi wake huyo zilichapishwa na Mama yake mwenyewe kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram, ambapo alipost picha ya gari hilo kisha akaandika 

"Alhamdulilaah kwa kila jambo mwanangu, Allah akuongezee zaidi na zaidi Ulipotoa Allah akupe kikubwa zaidi nakupenda sana nakuombea siku zote Hamisa Mobetto " ameandika Mama Mobetto 

Baada ya kupost picha hiyo ya kumshukuru na kumuombea mema mwanaye, Hamisa Mobetto na yeye ali-comment kwa kuandika 

"Nakupenda sana Mama yangu kipenzi, ningekua na uwezo ningekupa hata Dunia. Inshaallah Mwenyezi Mungu akijaalia Mjengo wetu Ukiisha, ntakununulia ile ingine unayoipenda zaidi" ameandika Hamisa Mobetto 

Wasanii wengine ambao waliwahi kuwazawadia wazazi wao vitu vya thamani ni Nandy, Dogo Janja ambao wote waliwazawadia wazazi wao nyumba