Thursday , 3rd Oct , 2019

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, awachalaza bakora wanafunzi 14, katika Shule ya Sekondari Kiwanja iliyopo Chunya mkoani Mbeya kwa madai ya kukutwa na simu za mkononi jambo ambalo ni kinyume na na utaratibu wa shule.

RC Chalamila amefikia maamuzi hayo wakati alipotembelea Shule hiyo ambapopia alipokea taarifa kutyoka kwa Mkuu wa shule hiyo ambaye aliwatuhumu wanafunzi hao kutumia simu shuleni hapo.

Wakati Mkuu Mkoa Chalamila akiwachapa wanafunzi hao, baadhi ya walimu katika shule hiyo walikuwa wakiomba RC huyo aongezewe viboko, ili aendelee kuwachalaza wanafunzi ambao kila mmoja alichalazwa viboko vitatu vitatu.

Mara baada ya kumaliza zoezi hilo, RC Chalamila amemtaka Mkuu wa Shule hiyo kuwachukulia hatua za kinidhamu wanafunzi hao ili iwefundisho kwao na wenzao waliopo shuleni hapo.