Tuesday , 1st Oct , 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameipongeza China kwa kuazimisha miaka 70 ya taifa hilo.

Rais Magufuli na Rais Xi Jinping

Rais Magufuli ametuma salamu hizo leo kwa watu wa China kupitia kwa Rais wa Taifa hilo Xi Jinping, ambapo amesema mataifa hayo yataendeleza ushirikiano na kulinda uhusiano kati yake uliodumu kwa miaka mingi.

Katika Salamu hizo ambazo Rais Magufuli amezitoa kupitia Twitter, baadhi ya maneno ameandika kwa Kichina kama, 祝贺习近平主席!祝贺全体中国人民 .

Maneno hayo yana maana kuwa, 'Hongera kwa Rais Xi Jinping na hongera pia kwa watu wote wa China'.

Leo Oktoba 1, 2019 China inasherekea kutimiza miaka 70 tangu taifa hilo liwe huru, huku likiwa ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua zaidi kiuchumi lakini pia likiwa ni taifa lenye watu wengi zaidi duniani wanaokadiliwa kufikia Bilioni 1.404.