Katika taarifa iliyotumwa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema Dkt. Athumani Kihamia ambaye alikuwa akishikilia nafasi hiyo sasa atapangiwa majukumu mengine.
Taarifa ya Ikulu imesema kuwa Wakurugenzi Watendaji walioteuliwa Ndaki Stephano Muhuli kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro.
Rehema Said Bwasi atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, Sheillah Edward Lukuba kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro.
Mohamed Mavura kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani, Ezekiel Henrick Magehema kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani Mbeya, Diana Sono Zacharia atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Hanji Godigodi atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe, Said H. Magaro atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora, Hawa Lumuli Mposi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoani Morogoro.
Godwin Justin Chacha atakuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro.
Aidha Rais Magufuli wahamisha eneo la kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro na kumpeleka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi Mkoani Singida, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani Bi. Advera Ndebabayo na kumpeleka kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.




