Thursday , 5th Sep , 2019

Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), limeishukuru Serikali na wadau wa soka nchini, wakiwemo mashabiki kwa ushirikiano ulioiwezesha timu hiyo kupata sare ugenini dhidi ya Burundi.

Mashabiki wa Taifa Stars baada ya mchezo wa jana huko Burundi.

Timu hiyo ya taifa ilipata sare ya 1-1 jana jioni kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2022 nchini Qatar.

Sare hiyo ilipatikana kwa goli la kusawazisha dakika ya 85, lililofungwa na Simon Msuva baada ya Tanzania kuwa nyuma kwa goli 1-0 kutoka dakika ya 81.

Baada ya mchezo huo kikosi cha Taifa Stars kinatarajiwa kuwasili Dar Es Salaam leo saa 11:35 jioni, kwa ndege ya Air Tanzania.

Mchezo wa marudiano utapigwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es salaam Septemba 8, 2019.