Saturday , 31st Aug , 2019

Miili ya marehemu watano waliofariki kwenye ajali ya lori la Dangote lililogongana na gari ndogo kisha kuwaka moto, imehamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuhifadhiwa na uchunguzi zaidi baada ya baadhi kushindwa kutambulika.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Onesmo Lyanga amesema miili ya watu watatu waliokuwa kwenye Lori la Dangote haijaweza kutambulika mara moja kutokana na kuteketea kwa moto.

Aidha Kamanda Onesmo amesema chanzo cha ajali bado kinachunguzwa hukuwa akiwaasa madereva kuwa makini.

Zaidi taarifa ya kamanda inaeleza hapo chini.