
Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC imesema kuwa maandalizi ya michezo ya jumuiya ya madola kwa vyama vya michezo nchini yamekua ya kusuasua pamoja na TOC kuwakumbusha mara kwa mara kwa njia mbalimbali
Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amesema kuwa awali walishaviandikia barua vyama vyote 8 kuomba taarifa za wachezaji wao wanaojiandaa kwa michezo ya jumuiya ya madola Glascow 2014 kuleta taaarifa hizo lakini hakuna chama kilichofanya hivyo
Wakati huo huo Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC imepongeza hatua ya serikali kupitia kwa wizara ya mambo ya nje kwa kutoa fulsa kwa wanamichezo mbalimbali watakaoshiriki michuano ya jumuiya ya madola kwenda kujiandaa nje ya nchi
Katibu mkuu wa TOC Filbert Bayi amevitakaka vyama hivyo vya michezo ya riadha, ngumi, judo na mpira wa meza kutumia fulsa hiyo ya waziri Membe kupeleka wachezaji vijana kwa faida ya baadae.