Waziri wa Maji na Umwagiliaji Profesa Jumanne Maghembe.
Wakiongea na East Africa Radio wakazi hao wamesema kwa kipindi kirefu wamekuwa wakipata adha ya maji jambo ambalo huwachukua muda za zaidi ya saa 6 kutafuta maji huku baadhi ya walina huduma hiyo wakilazimika kulipia gharama kubwa ambayo kwa wanakijiji wa kawaida hawezi kuimudu.
Afisa mtendaji wa kitongoji cha Olkushina amekiri kuwepo kwa tatizo la maji na miundombinu ya barabara ambapo amesema kwa sasa serikali inafanya kila liwezekanalo ili kupata ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo.
Wakati huo huo, leo ikiwa ni siku ya mwisho ya mitihani ya Darasa la saba nchini,Mkoa wa dodoma umesema unataraji kufanya vizuri mwaka huu kutoka nafasi ya tatu kutoka mwisho nafasi waliyoishika mwaka jana.
Akizungumza kabla ya kuanza mitahani hiyo hapo jana Afisa Elimu wa mkoa wa Dodoma Juma Kaponda amesema mwaka huu Ofisi yake imejipanga vyema kwa kushirikiana na walimu katika maandalizi ili kuweza kufanya vizuri mwaka huu.
Kaponda amesema hayo ya baada ya ziara ya kushtukiza ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dk. Shukuru kawambwa kuzitembelea baadhi ya shule za mkoa huo kushuhudia jinsi ya usimamizi wa mitihani hiyo inavyokwenda.